Maelezo Kutuhusu

Saeed Mohammed Al Ghandi & Wana (SMAG) ni mojawapo ya biashara za kimkoa yenye ubunifu mkuu zaidi na yenye makao yake makuu Dubai, Jumuiya ya Emirati za Kiarabu. SMAG inatoa usaidizi, sehemu na huduma pamoja na kuwa na vifaa vya kisasa zaidi na wafanyakazi wenye ujuzi ikiajiri watu 200. SMAG ni miongoni mwa Kundi la Magari la Al Ghandi; wakubwa wa magari wa UAE ambao wanaajiri zaidi ya watu 1,000 kwenye maeneo mbalimbali katika GCC na Afrika Mashariki. SMAG imepanuka kwa kiasi kikubwa miaka ya hivi karibuni kwenye maeneo mapya, ikiongeza nyayo zake mbali na GCC na kujumuisha Afrika Mashariki na Asia na kutoa huduma kamili kwa niaba ya watengenezaji bidhaa wanaosifika kimataifa. Kila modeli imejengwa kwa viwango madhubuti vya faraja, usalama na uimara, na kupitia mtandao wetu wa wauzaji, tunaweza kutoa vifaa vya ujenzi, mabasi, magari ya kufaa familia, magari ya kibosi, magari ya kibiashara, ufumbuzi wa kikodi, vifaa vya bahari, jenereta za nguvu, na mengi mengi zaidi.

Chini ya mwongozo wa kuhamasisha na uongozi wa H E Saeed Mohammed Al Ghandi, Kundi la Magari la Al Ghandi, lilifaulu kupata hati ya ISO 9001 kwa Usimamizi wa Ubora; ISO 14001 kwa Mfumo wa Usimamizi wa Kimazingira, OHSAS 18001 kwa Afya & Usalama wa Kikazi, ISO 10002 kwa Kuridhika Wateja na ISO 27001 kwa Usalama wa Habari wake. Hati hizi zimezawadiwa kwa kutambua kujitolea Al Ghandi kwa ubora wa kibiashara wa kutoa bidhaa na huduma za kiwango bora duniani kusaidia kuboresha mapitio ya wateja na kutoa mazingira mazuri zaidi ya kufanya kazi kwa wafanyakazi. Picha ya viwango.

Kundi la Magari la Al Ghandi liliibuka na wazo la Jumuiya ya Emirati ya Kiarabu kutoa soko linaoendelea kubadilika na bidhaa na huduma ya kiwango cha kimataifa. Tukiwa na wazo moja, tunasimama kidete kutimiza wazo letu – Kuwapa nguvu watu kwenye eneo zima kuhusisha na kuungana na kuboresha maisha ya wateja wetu kwa toleo bora zaidi liwezekanavyo la bidhaa, huduma na usaidizi. Tunajivunia kwa hilo. Tunaamini kuwa mawasiliano ya wazi na wafanyakazi, washiriki, waletaji na zaidi kuliko wote wateja wetu – ni msingi muhimu kwa mafanikio yetu. Matokeo yanathibitisha hili! Zuru www.alghandi.com kupata kujua zaidi kuhusu kundi hili.